MWAISABULA: WACHEZAJI WETU WAJIFUNZE KUCHEZA NA WENYEJI

Timu ya taifa ya Tanzania bara Kili Stars imeiaga michuano ya Challenge Cup baada ya kufungwa na wenyeji Ethiopia kwa changamoto ya mikwaju ya penati 4-3.

Kocha mzoefu soka Kenny Mwaisabula ‘Mzazi’ ametoa maoni yake juu ya mchezo huo ambao Kili Stars imejikuta ikiaga mashindano hayo kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Challenge.

“Tangu mwazo tulikuwa na akazi kubwa ya kufanya Ethiopia ambao tulidhani tungeweza kuwatoa baada ya kutoka nao sare kwenye mchezo uliopita, leo walibadilika wamecheza mchezo mzuri na sisi baada ya kupata goli tukawa-under rate na kuona tumeshashinda lakini mpira ni dakika 90 na unapocheza na mwenyeji chochote kianweza kutokea”, amesema Mwaisabula.

“Wamefanya makosa madogomadogo kama aliyofanya Kapombe na mwamuzi akamuadhibu na inabidi wachezaji wetu wajifunze wanapocheza na wenyeji wa mashindano ujue mchezo ni mgumu unacheza na mashabiki na referee anakuwa na tension kutokana na mashabiki walioko nje”.

“Sisi bado tunacheza mfumo ambao nadhani si mzuri sana kwasababu sasahivi naona timu yetu inajaza viungo wengi katikati ambao ni pure midfielders sio wale ambao wanauwezo wa kutoka na kukimbia pembeni na kurudi tena ndani na hili limekua ni tatizo kuanzia kwenye Kili Stars hadi taifa Stars kwa muono wangu mimi”.

Dakika 90 za mchezo huo zilimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana goli 1-1 na kuufanya mchezo huo kuamuliwa kwa matuta. Goli Stars lilifungwa na John Bocco ‘Adebayor’ lakini Ethiopia walisawazisha goli hilo kwa mkwaju wa penati baada ya Shomari Kapombe kumwagusha mchezaji wa Ethiopia kwenye eneo l;a hatari”.

Mchezo wa awali ulishuhudiwa Uganda ikifanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kwa kuifunga timu ya Malawi kwa magoli 2-0 kwenye mchezo huo wa robo fainali ya kwanza.