Rais Dkt.Magufuli ameagiza Fedha za sherehe za uhuru kutumika kuipanua barabara ya Ally Hassani mwinyi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ameagiza fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shamrashamra za sherehe za uhuru kiasi cha shilingi bilioni nne sasa zitumike kujenga kupanua barabara ya Ally Hassan Mwinyi kutoka eneo la Moroco hadi Mwenge jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupunguza kero ya foleni.

Mapema asubuhi rais Dr Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa China hapa nchini Dr Lu Youquing mazungumzo yaliyolenga kutoa taarifa kwa Dr Magufuli juu ya mkutano kilele wa sita wa jukwaa la ushirikiano wa China na Afrika yaani Forum for China Africa Co-operation utakaofanyika nchini Afrika ya Kusini kati ya tarehe 4 na 5 mwezi December mwaka huu jijini Johnesburg mkutano unaodaiwa wa manufaa makubwa kwa Afrika Tanzania ikiwenmo.

Kisha, rais Dr Magufuli akafanya mazungumzo na balozi wa Korea ya Kusini anayemaliza muda wake hapa nchini Chung Il ambaye ametaka kuharakishwa kwa ujenzi wa daraja Salender litakalokuwa na urefu wa km 6.3 pamoja na maingilio yake kutoka eneo la Boco Beach hadi hospitali ya Aghakhan jijini Dar es Salaam na akimhakikishia rais uwepo wa fedha hizo, ambapo rais amemshukuru na kumhakikishia ushirikiano baina ya Tanzania na Korea ya Kusini katika harakati za kimaendeleo.

Baadae rais Dr Magufuli akakutana na kufanya mazungumzo na aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof Ibrahimu Haruna Lipumba Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Prof Lipumba amempongeza rais Dr Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano lakini pia kwa hotuba nzuri iliyojaa uzalendo ya uzinduzi wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku rais akimpongeza Prof Lipumba kwa msimamo wake thabiti wa kupinga ufisadi.

Aidha, katika hatua nyingine rais Dr John Pombe Magufuli ametoa agizo kwa mtendaji mkuu wa wakala wa barabara nchini Tanroad Mhandisi Patrick Mfugale kuanza mara moja upanuzi wa barabara ya Ally Hassan Mwinyi kutoka eneo la Mwenge hadi Moroco kwa kutumia fedha hizo zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya kugharamia shamrashamra za sherehe za uhuru wa Tanganyika ambapo kiasi cha shilingi bilioni zilizookolewa zitatumika.

Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita nne nukta tatu sasa ujenzi wake umeamriwa kuanza kutekelezwa mara moja kwa kutumia fedha hizo jambo ambalo litapunguza msongamano wa magari katika barabara hiyo huku wananchi nao wakitoa maoni yao kuhusu uamuzi huo.