Bomoa bomoa Yaikumba Morogoro

Ni kwa wakazi waliojenga pembezoni mwa bwawa la Mindu..

Halmashauri ya Manispaa ya morogoro ikishirikiana na mamlaka ya maji safi na maji taka mkoa wa Morogoro MORUWASA wameendesha zoezi la ubomoaji wa majengo yote yaliyopo pembezoni mwa bwawa la Mindu.

Channel Ten imeshuhudia zoezi la bomoabomoa likiendelea katika vibanda vya wafanyabiashara na wavuvi vilivyopo karibu na bwawa hilo ambavyo inadaiwa vimejengwa kinyume cha sheria huku kukuwa na biashara ya vileo kando na bwawa hilo.

Baadhi ya wafanyabiashara na wavuvi katika bwawa hilo wamelalamikia zoezi hilo kwa madai kuwa limewaathiri kwa kiasi kikubwa huku wakiitupia lawama manispaa ya morogoro kwa kubomoa majengo yasiyohusika katika zoezi hilo ikiwemo choo ambacho kilikuwa kikitumika na wavuvi hao.