Mastaa waliofanya siri kuficha mimba, watoto 2015

   Jenifer Kyaka.

MIONGONI mwa vioja vilivyotikisa mwaka 2015 ni kitendo cha baadhi ya mastaa wa filamu Bongo kuyapiga chenga madai ya kubeba mimba na kuzaa huku wengine wakificha watoto wao, kwa kutotaka waonekane sura pasipo kuwa na sababu za msingi.
Katika makala haya, yanachambua baadhi ya mastaa waliofanya hivyo;

AUNT EZEKIEL
Staa huyu asiyechuja, gumzo kubwa lilianza baada ya kupewa ujauzito na dansa wa staa wa Bongo Fleva, Diamond aitwaye Moze Iyobo.

AUNT EZEKIEL.
Katika kipindi chote cha ujauzito wake, Aunt alikuwa akijianika lakini tafrani ilizuka baada ya kujifungua na kuanza kumficha sura mtoto huyo kukwepa macho ya watu na hata alipokuwa akimuanika kwenye mitandao ya kijamii bado aliendelea kumficha sura.

ODAMA
Jina lake kwenye hati ya kusafiria ni Jenifer Kyaka. Staa huyu naye ni miongoni mwa mastaa ambao jambo la kuwaanika watoto wao limekuwa ishu kubwa.

Tangu ajifungue mtoto wake mwaka jana, hadi sasa hajathubutu hata siku moja kumuanika na hata mzazi mwenziye hajulikani.

MARY MAWIGI
Mwanadada huyu tangu kipindi cha ujauzito wake alikuwa akikanusha kuwa yeye ni mama kijacho, mwisho wa siku alipojifungua alikiri kuwa amezalishwa na mwanaume ambaye dini zao ni tofauti japo hakuwa tayari kumuanika na kufikia uamuzi wa kubadili dini kutoka Ukristo na kuingia Uislam huku wakiwa kwenye mikakati ya kufunga pingu za maisha.

SANDRA
Anajulikana kama Salama Salmini ‘Sandra’ ni miongoni mwa watu waliokanusha kipindi cha ujauzito hadi muda mwingine kugeuka mbogo kwa sababu tu ya kuulizwa ishu hiyo.

Kuna kipindi alikuwa akichenga kuonana na mapaparazi kwa kuhofia kupigwa picha ujauzito wake, licha kwamba ulikuwa ni wa tatu. Hata hivyo, baada ya kujifungua aliweka wazi kuwa alikuwa mjamzito na anafurahi kufikia ndoto yake ya kupata mtoto wa kike.

SAJENTI
Kama mwenyewe anavyopenda kujiita ‘supa staa’ ni miongoni mwa wasanii ambao hakuwa tayari kuanika ujauzito wake na hata alipojifungua bado ilikuwa ishu kukiri.

Ilifikia hatua hata siku ya arobaini ya mwanaye hakutaka kuweka wazi jambo hilo kwa mapaparazi kuhofia kupigwa picha mwanaye. Hata hivyo, baada ya kuficha sana, picha za mtoto wake zilikuja kufumwa na kubakiwa na aibu.