Wanawake 3 kutoka Pakistan wajiunga na IS

Polisi nchini Pakistan wanasema wanawake watatu wameondoka mji wa Lahore na kwenda kujiunga na wapiganaji wa Islamic State nchini Syria.

Hiki ndicho kisa cha kwanza cha wanawake kutoka nchini Pakistan kuondoka na kwenda maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji hao.

Wanawake hao, pamoja na watoto wao, wanadaiwa kuondoka na kuvuka mpaka hadi Iran kabla ya kuendelea na safari hadi Syria.

Siku za awali, Pakistan imekana kuwepo ka wanachama wa IS au wahudumu wao nchini humo.
Lakini mapema wiki hii maafisa wa usalama walisema walifanikiwa kuvunja kundi la wanachama wa IS karibu na mji wa Lahore.

Habari katika gazeti moja linasema mmoja wa wanawake walioenda kujiunga na IS alikuwa mwalimu mkuu wa shule ya Kiislamu mjini Lahore.