ASLAY WA YAMOTO BAND ABWAGA MANYANGA KWA VIDEO QUEEN HUYU

Msanii wa kundi la Yamoto Band, Aslay Isihaka ametangaza kuwa yupo single.

Kabla ya hapo, Aslay aliwahi kuweka hadharani uhusiano wake na video model aitwaye Tessy Chocolate.

Hata hivyo siku za hivi karibuni muimbaji huyo aliacha kupost picha za mrembo huyo kwenye mtandao wa Instagram kiasi cha watu kuanza kuhisi kuwa mambo yameharibika.

Wiki hii aliiambia E-Newz ya East Africa Television kuwa kwa sasa hana mahusiano na binti yoyote.
Alisema kuhusiana na kinachoendelea katika upande wa mahusiano yake, hawezi kukizungumzia kwa sasa mpaka atakapoamua kuweka wazi nini kilitokea. Pia Aslay alishindwa kuzungumzia uvumi uliopo kuwa amemuacha msichana huyo baada ya kupata ujauzito.