Asali ni chakula cha kimiminika kitamu kinachotengenezwa na nyuki. Asali imekuwa ikitumika kwa karne nyingi kama chakula na dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali.
Asali ni mchanganyiko wa sukari za wanga, kampaundi mbalimbali kama madini na vitamini pamoja na maji.
Asali ina sukari za:
Sukari za aina ya fruktozi na glukozi ndio huleta utamu mzuri wa asali. Asali ina kiasi kidogo sana cha protini, vitamini B na C, madini ya Kalsiamu, fosfotasi, chuma, zinki na potasiamu. Asali haina mafuta kabisa.
Faida za Kiafya
Matumizi ya asali yana faida nyingi kwa afya yako. Unaweza kutumia asali badala ya sukari ya kawaida kwenye vinywaji kama chai n.k.
Kutibu allergy za vumbi
Asali hutumika kutuliza allergy hasa zinazotokana na vumbi.
Hutumika Kutibu vidonda
Vidonda kutokana na kuungua moto au kuumia vinaweza kutibiwa kwa kutumia asali. Asali huzuia bakteria kuota kwenye kidonda na hivyo kidonda hufunga vizuri.
Kutibu saratani
Asali inaaminika kuwa na uwezo wa kuua seli zenye saratani, bado tafiti zinaendelea kufanyika juu ya uwezo wa kutibu saratani.
Kutibu kikohozi
Asali imekuwa ikitumika kutibu kikohozi hasa kwa watoto. Kunywa asali kwenye kijiko au changanya na maji ya moto kisha kunywa.
Kuimarisha kinga ya mwili
Huimarisha afya ya ngozi na kuondoa harara na chunusi.
Tahadhari ya Matumizi ya Asali

- Fruktozi 38.2%
- Glukozi 31.3%
- Maltozi 7.1%
- Sukrozi 1.3%
- Maji 17.2%
- Kampaundi nyingine (Vitamini, Madini na Protini) 3.2%
Sukari za aina ya fruktozi na glukozi ndio huleta utamu mzuri wa asali. Asali ina kiasi kidogo sana cha protini, vitamini B na C, madini ya Kalsiamu, fosfotasi, chuma, zinki na potasiamu. Asali haina mafuta kabisa.
Faida za Kiafya
Matumizi ya asali yana faida nyingi kwa afya yako. Unaweza kutumia asali badala ya sukari ya kawaida kwenye vinywaji kama chai n.k.
Kutibu allergy za vumbi
Asali hutumika kutuliza allergy hasa zinazotokana na vumbi.
Hutumika Kutibu vidonda
Vidonda kutokana na kuungua moto au kuumia vinaweza kutibiwa kwa kutumia asali. Asali huzuia bakteria kuota kwenye kidonda na hivyo kidonda hufunga vizuri.
Kutibu saratani
Asali inaaminika kuwa na uwezo wa kuua seli zenye saratani, bado tafiti zinaendelea kufanyika juu ya uwezo wa kutibu saratani.
Kutibu kikohozi
Asali imekuwa ikitumika kutibu kikohozi hasa kwa watoto. Kunywa asali kwenye kijiko au changanya na maji ya moto kisha kunywa.
Kuimarisha kinga ya mwili
Huimarisha afya ya ngozi na kuondoa harara na chunusi.
Tahadhari ya Matumizi ya Asali
- Baadhi ya maua ambayo nyuki hutumia kutengeneza asali yanaweza kuwa na sumu.
- Asali isitumike kwa watoto wachanga kwani wana hatari ya kupata ugonjwa wa botulism.
- Watu wenye kinga dhaifu sana hawashauriwi kutumia asali kwa sababu ya hatari ya maambukizi ya bakteria au fangasi.