F FAIDA ZA NDIZI MWILINI | Muungwana BLOG

FAIDA ZA NDIZI MWILINI

FAIDA ZA NDIZI
Ndizi mbivu ni tunda linalotumika sana kama mlo sehemu mbalimbali duniani. Ni tunda ambalo ni tamu na lenye virutubisho mbalimbali na muhimu kwa mwili.

Baadhi ya faida za ndizi kiafya ni kusaidia moyo kufanya kazi vizuri, kupunguza uwezekano wa kupata saratani na pumu. Ndizi ni chanzo kizuri cha madini ya Potasiamu.

VIRUTUBISHO VILIVYOMO KWENYE NDIZI
Ndizi ya wastani ina uzito wa kama gramu 126O. Ina nishati kiasi cha kalori 110, gramu 30 za wanga na gramu 1 ya protini. Ndizi hazina fati, lehemu (cholesterol) au madini ya Sodiamu.

Ndizi zina virutubisho  vifuatavyo;

  1. Vitamini B6 – 0.5 mg
  2. Manganizi- 0.3 mg
  3. Vitamini C – 9 mg
  4. Potasiamu – 450 mg
  5. Kambakamba- 3g
  6. Protini – 1 g
  7. Magneziamu – 34 mg
  8. Madini ya Foliki- 25.0 mcg
  9. Riboflavin – 0.1 mg
  10. Niacin – 0.8 mg
  11. Vitamini A – 81 IU
  12. Madini ya chuma – 0.3 mg
  13. FAIDA ZA NDIZI KIAFYABananas


Kushusha Shinikizo la Damu
Ndizi zina madini ya Potasiamu kwa wingi ambayo husaidia kulegeza mishipa ya damu na hivyo kupunguza shinikizo la damu au presha (blood pressure). Pia ulaji wa madini ya potasiamu kwa wingi hupunguza hatari ya kufa kutokana na magonjwa mbalimbali.

Kupunguza Uwezekano wa Kupata Pumu (Asthma)
Ndizi zinadhaniwa kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa pumu kwa watoto. Ulaji wa ndizi moja kila siku kwa mtoto unaweza kupunguza hatari ya pumu.

Kupunguza Hatari ya Kupata Saratani
Ndizi ni chanzo kizuri cha vitamini C ambayo husaidia kuondoa sumu kwenye mwili ambazo husababisha saratani kutokea. Pia kambakamba (fibers) zinazopatikana kwenye ndizi kwa wingi husaidia kuondoa sumu kwenye utumbo zinazoweza kuchangia saratani ya utumbo.

Ufanyaji Kazi wa Moyo
Madini ya Potasiamu, vitamini C na B ambayo hupatikana kwa wingi kwenye ndizi huwezesha moyo kufanya kazi vizuri. Ulaji wa vyakula vyenye Potasiamu kwa wingi na Sodiamu kidogo kama ndizi hupunguza hatari ya magonjwa kama shambulio la moyo, kiharusi na shinikizo la damu la kupanda.

Kutibu Kuharisha
Kuharisha hupoteza madini mengi hasa ya Potasiamu. Ulaji wa ndizi utakusaidia kurudisha madini haya mwilini mwako.

Kuimarisha Kumbukumbui 
Ndizi zina tryptophan, aina ya protini ambayo huusika kwenye ufanyaji kazi wa kumbukumbu. Ulaji wa ndizi kwa windi inaweza kukusaidia kuongeza uwezo wako wa kufikiri.

 TAHADHARI YA MATUMIZI YA NDIZI
Matumizi ya ndizi huweza kuleta madhara kwa watu wenye matatizo hasa ya figo au wanaotumia dawa kama beta blockers kama labetalol. Ndizi zina madini mengi ya Potasiamu, hivyo kwa watu wenye matatizo ya figo hushindwa kutoa Potasiamu na kusababisha madini haya kujaa kwenye damu ambayo itaathiri afya ya mgonjwa.