IDARA ya uhamiaji Mkoa wa Geita imekamata wahamiaji 28

IDARA ya uhamiaji Mkoa wa Geita imekamata wahamiaji 28 kutoka nchi za Burundi na Rwanda walioingia nchini kinyume cha sheria kwa ajili ya kufanya vibarua.

Afisa uhamiaji Mkoa wa Geita Charles Washima amesema wahamiaji hao wamekamatwa katika kata za Nkome na Igate walikokuwa wakifanya shuguli za kulima.

Mbali ya wahamiaji hao 28 raia wawili wa Tanzania waliokuwa wenyeji wa wageni hao pia wamekamatwa na kufikishwa mahakamani.

Mkoa wa Geita unakabiliwa na idadi kubwa ya wahamiaji haramu, wengi wao kutoka nchi za Burundi na Rwanda wanaoingia nchini kwa ajili ya kufanya kazi za kilimo wengi wao wakisaidiwa kuingia nchini na watanzania ili kuwapatia ajira.