MSANII ROSE NDAUKA AJA NA TEAM YAKE KWA WASANII CHIPUKIZI

Rose Ndauka amesema anapenda muziki ndio maana akaamua kuanzisha kitengo cha ‘Rosie Family’ ili kusaidia wasanii waliokosa msaada.

Muigizaji huyo ambaye pia ni mfanyabiashara, ameiambia Bongo5 Ijumaa hii kuwa mpaka sasa ana wasanii 10 anaotaka kuwasaidia.

“Kwenye moyo wangu ndani ukinipasua napenda sana entertainment na moja ya burudani nayopenda ni muziki, napenda kusikiliza muziki, napenda kucheza,” alisema Rose.

“Nikikutana na kipaji ambacho kinafanya kizuri sikiachi, kwahiyo mimi kama dada nahisi kwamba naweza nikabeba majukumu. Kwahiyo nahisi kwamba nina jukumu la kumchukua yule msanii na kumfikisha sehemu fulani. Kwahiyo kundi langu linaitwa Rosie Family ni familia hatuiti kundi, kuna wasanii kumi na wote nimepanga kila mwenye juhudi ndiye atakayeanza kutoka,” alisema Rose.

Aidha muigizaji huyo alidai katika kipindi cha nyuma aliwahi kurekodi nyimbo mbili na kuzitoa lakini hazikufanikiwa kufanya vizuri.