Mwezi wa 1 tu serikali imetoa Sh bilioni 318.46 kulipa miradi ya ujenzi, umeme, barabara na mifuko ya hifadhi

Serikali imesema kwa mwezi January tu imefanikiwa kutoa shilingi bilioni 318.46 kulipia miradi ya ujenzi, umeme, barabara na mifuko ya hifadhi.

Katibu mkuu wizara ya fedha na mipango Dr.Servecius Likwelile amesema fedha hizo zinatokana na mapato ya ndani pekee bila kutegemea za wahisani.

Naye gavana wa benki kuu ya Tanzania Profesa Benno Ndulu amesema kwa sasa uchumi umeanza kuimarika kutokana na kuimarika ukusanyaji wa mapato huku matumizi yakidhibitiwa.

Kwa upande wake kaimu kamishina mkuu wa mamlaka ya mapato-TRA  Alphayo Kidata amesema mamlaka yake inatarajiwa kuvuka lengo la ukusanyaji kodi kwa mwezi huu kutokana na kufanikiwa kuziba mianya mingi ya ukwepaji.