Mzee Yusuf, Vanessa Mdee Wafunika Dar Live

Mfalme wa Taarabu, Mzee Yusuf na mrembo anayetamba kwenye Muziki wa Bongo Fleva kwa sasa, Vanessa Mdee wameweka historia ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live, usiku wa jana baada ya kuachia bonge la shoo ya wimbo wao unaokwenda kwa jina la Mashallah.

Wawili hao walifanya shoo hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa albamu ya kumi na moja ya Jahazi yenye nyimbo saba inayokwenda kwa jina la Kaning’ang’ania huku wakisindikizwa na Kundi la Taarabu la Ogopa Kopa linaloongozwa na Malkia Khadija Kopa.

Vanessa Mdee aliyepanda jukwaani na Mzee Yusuf sambamba na kundi zima la Jahazi walipiga shoo ya kufa mtu na kuwaacha mashabiki wa muziki huo vinywa wazi kwa mara ya kwanza wakishuhudia ladha ya muziki tofauti kutoka kwa wawili hao.