Serikali imechukua hatua za dharura za kuchimba mabwawa ya uhifadhi wa maji

Serikali imechukua hatua za dharura za kuchimba mabwawa ya uhifadhi wa maji, ili kuokoa barabara ya Dodoma ñ Dar es Salaam isikatike, kufuatia mvua zinazoendelea sasa kuleta mafuriko na kumomonyoa barabara hiyo.

Uamuzi huo wa haraka umefikiwa wakati Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bw. Edwin Ngonyani alipotembelea eneo la Kibaigwa na kujionea uharibifu mkubwa wa barabara uliosababishwa na maji yanayotoka katika milima ya  kiteto mkoani Manyara.

Kuja kwa maamuzi hayo, kunafuatia ukweli uliotolewa na wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo, kama Bw. Bakari Ali alivyomweleza naibu waziri uwepo wa mabwawa ambayo kwa sasa yamejaa udongo.

Hawali mkandarasi anayerekebisha eneo lililoharibika, Thobias Kyando alikuwa na wazo la kuchepusha maji yanayoingia barabarani, lakini ikaonekana kuwa haitakuwa suluhisho la kudumu, na mhandisi wa TANROADS Eng. Emmanuel Tarimo, akahidi  kuwasiliana na watu wa maji ili waweze kuchimba mabwawa.