Wakazi Same wakataa agizo la serikali kufyeka miti ya dawa za kulevya aina ya Mirungi

Wakazi wa wilaya ya Same wanaoishi karibu na hifadhi ya msitu wa Shengena wamepinga agizo la serikali linalowataka kufyeka miti ya asili inayo julikana kwa jina la Izengo kwa madai kuwa miti hiyo ndiyo inayo toa madawa ya kulevya aina ya Mirungi huku wao wakidai kuwa miti hiyo aina mahusiano na dawa za kulevya na kwamba kukatwa kwa miti hiyo kuta changia uharibifu mkubwa wa mazingira katika msitu wa Shengena kwakuwa sehemu kubwa ya misitu huo umeenea miti ya aina hiyo.

huu ndio Mti wa mirungi..

Kauli hizo zimesemwa na wakazi wa tarafa nne za wilaya ya Same ambao wamepata agizo la serikali la kuwataka kufyeka miti hiyo iliyo katika maeneo ya kuzunguka makazi yao kwa madai kuwa ni dawa za kulevya aina ya Mirungi na wao kudai kuwa ni miti ya asili inayo julikana kama Izengo na siyo Mirungi kama inavyo daiwa lakini pia kufyekwa kwa miti hiyo kutachangia uharibifu mkubwa wa mazingira katika hifadhi ya msitu wa Shengena.

Kwa upande wao watalam wa mazingira kutoka taasisi zinazo jihusisha na uhifadhi wa mazingira wamesema serikali inapaswa kuangalia kwa mapana maamuzi yake na kutoa elimu ya kutosha kwa jamii endepo imegundua kuwa miti hiyo inamadhara lakini ikumbuke kuwa wilaya ya Same imewai kukumbwa na maafa mengi yaliyo sababishwa na uharibifu wa mazingira hivyo kuna aja ya kuulinda msitu wa Shengena kwa manufaa ya umma.

Ripota wetu alimtafuta meneja wa wakala wa misitu kanda ya kaskazini Cathbeth Mafupa ambaye amesema ni kweli miti hii ni ya asili lakini inamadhara kwa binadamu wanayo tumia kama dawa za  kulevya na serikali haina mpango wa kuikata miti iliyo ndani ya msitu bali ni ile iliyo kwenye makazi ya binadamu ambayo wameipanda kwa makusudi ya kutumia kama dawa za kulevya ili kuepusha madhara kwa watumiaji.