F Dawa mbadala 10 zinazotibu Kisukari | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Dawa mbadala 10 zinazotibu Kisukari

1. UWATU

 Katika makala hii tutaangalia dawa mbadala mbalimbali 10 zinazotibu ugonjwa wa kisukari. Labda utakuwa unajiuliza, Je kisukari kinatibika? Ndiyo kisukari kinatibika. Mhimu ni upate tiba mbadala au tiba asilia ambazo ni sahihi. Ili kujifunza mengi na kufahamu mengi kuhusu ugonjwa wa kisukari, kwamba kisukari ni nini? Au ugonjwa huu hutokeaje mwilini, Nakushauri usome kwanza makala hii => Fahamu kuhusu Ugonjwa wa Kisukari

Umakini unahitajika sana hasa kwa mgonjwa yule ambaye ameanza kutumia dawa za hospitalini kila siku. Nakushauri usianze kuzitumia hizi dawa moja kwa moja ukiwa peke yako bila uangalizi wa karibu wa daktari au mganga wa tiba za asili.

Twende sasa tuzichambuwe hizi dawa moja baada ya nyingine kama ifuatavyo;



Dawa mbadala 10 zinazotibu Kisukari

1. UWATU

Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa uwatu unao uwezo mkubwa katika kutibu kisukari. Uwatu huzisisimua seli katika kongosho kitendo kinachofanya uzalishwaji wa insulini kuongezeka. Maajabu haya ya uwatu yanasemekana kufanyika kutokana na uwatu kuwa na asidi amino mhimu sana ijulikanayo kama ‘4-hydroxyisoleucine’. Miaka mingi kabla hata ya huu utafiti kufanyika, uwatu umekuwa ukitumika kama moja ya dawa bora kabisa za asili katika kutibu kisukari.

Namna ya kuutumia Uwatu kujitibu kisukari

  • Chota mbegu za uwatu vijiko 4 na uziloweke katika maji robo lita kwa usiku mmoja. Asubuhi ponda ponda hizo mbegu za uwatu ndani ya maji kisha zichuje na upate maji yake. Kunywa maji haya kila siku asubuhi kwa muda wa miezi 2.
  • Chukuwa uwatu ya unga vijiko vikubwa 2 na uweke ndani ya maziwa au maji ya uvugu uvugu robo lita, koroga vizuri na unywe kila siku kutwa mara 2 kwa miezi 2.
  • Chukuwa gramu 100 za mbegu za uwatu na gramu 50 za binzari manjano. Unaweza kuongeza kiasi kidogo cha pilipili manga nyeupe kwenye mchanganyiko huu. Ongeza kijiko 1 cha mchanganyiko huu wote katika maziwa robo lita na unywe kutwa mara 2 kila siku.
  • Unaweza pia kuongeza uwatu ya unga katika unga wako unaotumia kutengenezea mkate au hata chapati.


 2. MDALASINI