Jeshi la Polisi laua majambazi watatu katika majibizano ya risasi mkoani Arusha

Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limewaua kwa risasi watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi na kukutwa na bunduki moja aina ya AK 47 ikiwa na risasi kumi na nane milipuko ishirini na saba sale za jeshi la wananchi wa Tanzania na bendera inayodaiwa kutumiwa na kikundi cha Al Shababy katika tukio lililotokea eneo la Engosheraton Sinoni jijini Arusha.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Libaratus Sabas amesema jeshi la polisi lilipata taarifa ya uwepo wa majambazi hao kutoka kwa wasamariawema wakitaka kufanya tukio na baada ya kufika katika eneo la tukio watu hao walianza kurusha risasi kwa askari lakini askari waliwashinda nguvu na kufanikiwa kuuwa majambazi watatu ambapo mmoja akifaamika kwa jina la Athumani Ramadhani.

Aidha kamanda Sabas amevitaja vifaa pamoja silaa zingine walizi kutwa nazo majambazi hao ikiwa ni pamoja na pikipiki simu na vingine mapanga na visu kama anavyoeleza na baadhi ya wananchi wakilitaka jeshi la polisi kuendelea kuzibiti ongezeko la silaa na kuchunguza mahali panapo toka silaa hizo za kijeshi ambazo zimeenea katika maeneo mengi ya raia.