Kamatakamata ya wafanyabiashara wanaofanyabiashara katika baadhi ya maeneo ya kariakoo yasiyo rasmi

Kamatakamata ya wafanyabiashara wanaofanyabiashara katika baadhi ya maeneo ya kariakoo yasiyo rasmi  imeendelea ambapo askari wa FFU pamoja na askari kanzu wameendesha zoezi hilo katika maeneo hayao.

Operesheni hiyo imeshika kasi baada ya wafanyabishara hao waliokuwa wakipanga bidhaa katika barabara mpya za mwendo kasi mtaa wa msimbazi kumshambulia na kusababisha kifo cha mtu mmoja kwa madai ya kukanyaga bidhaa walizopanga chini.

Baadhi ya wananchi katika eneo hilo wameunga mkono Operesheni hiyo ya kuwaondoa wafanyabiashara hao kwa madai kuwa wamekuwa chanzo cha Vibaka na waporaji kutokana bidhaa wanazotandaza chini na hivyo kusababisha Usumbufu mkubwa kwa wapita njia.

Hata hivyo baadhi ya wafanyabishara wamelalamikia zoezi hilo baada ya bidhaa zao kuchukuliwa.