Ugonjwa wa Kipindupindu umeendelea kuwa tishio nchini huku mikoa 12 ikiwa inaongoza


Ugonjwa wa Kipindupindu umeendelea kuwa tishio nchini huku mikoa 12 ikiwa inaongoza kwa kuwa na wagonjwa wengi na kutoa  tahadhari  kwa wananchi kuzingatia usafi na kanuni zote za afya iki kujikinga na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Naibu waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Dr Khamis Kigwangwala amesema kuwa mpaka kufikia  february 28 2016 jumla ya wagonjwa 16,825 wameripotiwa kuugua kipindupindu huku watu  258 wakipoteza maisha

Aidha Dr Kigwangwala ameitaja mikoa inayoongoza kuwa na wagonjwa wengi  wa kipindupindu kuwa ni mkoa wa Mara wagonjwa 125,Dodoma wagonjwa 87,Iringa wagonjwa 64,Mwanza wagojwa 59,Morogoro wagonjwa 44,Mbeya wagonjwa 29,Dar es salaam wagonjwa  25,Arusha wagonjwa 18,Kigoma wagonjwa 8,Rukwa wagonjwa 6,Simiyu wagonjwa 6 huku singida ikiwa na wagonjwa 2.

Naibu Waziri huyo ameendelea kusema kuwa licha ya Wizara kuendelea kupambana na ugonjwa huo lakini juhudi hizo zimekuwa zikikwamishwa na  baadhi ya wataalamu wa afya pamoja na wanajamii ambao wamekuwa wakiwaficha wagonjwa wa kipindupindu na kutoa taarifa ya wagonjwa isiyo rasmi na kuahidi kuwashughulikia wataalam hao.

Dr Kigwangwala ameitaka jamii kuungana na halmashauri,mikoa pamoja na Wizara katika juhudi za kupambana na Kipindupindu kwa kuzingatia kunywa maji yaliyo safi na salama,kuepuka kula chakula kilichoandaliwa katika mazingira hatarishi,kutumia vyoo na kutojisaidia ovyo katika vyanzo vya maji vya mito,maziwa na mabwawa.