Wanafuzi 106 wa kidato cha sita shule ya sekondari mkoani Ruvuma wameandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa

Wanafuzi 106 wa kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Namabengo wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wameandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa wakilalamikia vitendo vya udhalilishaji vinavyodaiwa kufanywa makamu mkuu wa shule hiyo.

Mwalimu huyo anadaiwa kutoa vitisho na lugha za matusi kwa wanafunzi,kuchapwa viboko visivyo na idadi,kuingia kwenye bweni la wanafunzi wa kike nyakati za usiku bila kuongozana na matroni na kuwalazimisha kutaka kufanya mapenzi pamoja na kuwazuia wanafunzi wa kike kulala bwenini.

Kutokana na malalamiko ya wanafunzi hao walitaka kwenda kumwona mkuu wa mkoa ili aweze kusikiliza na kuzipatia ufumbuzi kero zao juhudi za kutaka kuonana na mkuu huyo wa mkoa ziligonga mwamba wakati wameshatembea kwa miguu kilomita Zaidi ya 16 kabla ya kufika Songea mjini ambako askari polisi wakiongozwa na mkuu wa polisi wilaya ya Namtumbo kuwazuia wasiendelee na maandamano.

Wanafunzi hao walikutwa kijiji cha Mlete  kilicho nje kidogo ya manispaa ya Songea ambapo askari polisi waliwaamuru wasimame ndipo mkuu wa polisi wilayani humo aliwataka waeleze sababbu za kufanya maandamano bila kibali,wanafunzi hao walimweleza kuwa kila mtu anahaki ya kuongea kwa kuwa walishatoa malalamiko yao kwa mkuu wa shule lakini hayakusikilizwa hivyo waliona vema wakakutane na mkuu wa mkoa labda ataasikiliza.

Baada ya viongozi hao kusikiliza malalamiko ya wanafunzi waliwataka warudi shuleni ili wakatoe maamuzi mbele ya wanafunzi wote pamoja na walimu jambo ambalo wanafunzi walikubali na kusitisha maandamano na kurudi shuleni.