Askari Polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia ( FFU ) mkoani Mwanza wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wakazi wa mtaa wa Mwananchi - Susuni kata ya Mahina jijini humo baada ya kufunga barabara kuu ya Mwanza – Musoma kwa kuweka vizuizi vya mawe kufuatia mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya St. Angeline Mase Magabe Chacha kugongwa na daladala wakati akienda shuleni.
Tukio la kufunga barabara hiyo limetokea jana majira ya saa 12 jioni ambapo ITV ilishuhudia wakazi wa mtaa huo wengi wao wakiwa ni vijana, wakiwa katika hekaheka ya kupanga mawe makubwa barabarani huku wengine wakijaribu kuyaponda kwa mawe magari ambayo yalitaka kutumia barabara hiyo, jambo lililowalazimu baadhi ya madereva ambao walikuwa wakielekea nyakato na igoma kuamua kutumia barabara ya Makongoro – Nyasaka na kutokea Buzuruga.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwananchi – Susuni, Misarambo Elisamia amemuomba meneja wa wakala wa barabara ( TANROADS ) mkoani mwanza kujenga tuta au kuweka alama za pundamilia ili kuokoa maisha ya watumiaji wa barabara hiyo.
Wakazi wa mtaa wa Susuni kata ya mahina,kilio chao ni ajali za mara kwa mara zinazotokea katika barabara hiyo na kupoteza maisha ya watu.
Bi. Pili Mase ni mama mzazi wa marehemu mase magabe chacha aliyekuwa na umri wa miaka kumi, ambaye alifia katika hospitali ya rufaa Bugando wakati akipatiwa matibabu baada ya kugongwa na HIACE iliyokuwa ikitoka igoma kuelekea mjini,masikitiko yake ni kuhusiana na huduma duni za matibabu katika hospitali hiyo.