CCM Yawataka Wafanyabiashara Kupuuza kauli za Wanasiasa kuwa Rais Magufuli Analengo la Kuwakomoa.

Chama cha Mapinduzi kimewataka watanzania kupuuza kauli za baadhi ya wanasiasa zinazodai kuwa rais Magufuli analengo la kuwakomoa wafanyabiashara na kinazieleza kauli hizo kuwa ni za uchochezi kwakuwa serikali ya awamu ya tano haina tatizo na wafanyabiashara na watumishi waadilifu bali wanaolihujumu taifa kwa manufaaa binafsi.

Kauli hiyo ya chama imetolewa na msemaji mkuu wa CCM Christopher Ole Sendeka wilayani Simanjiro alipokuwa akizungumza na wananchi wanachama wafuasi wa CCM na viongozi wa mila katika kata ya Shambarai.

Kwa upande katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha Shabani Mdoe amewataka wananchi kuwa makini na viongozi wasio waadilifu huku mkuu wa wilaya ya Simaniro Mahamoud Kambona akiwata viongozi wa mila kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo.

Katika mkutano huo viongozi wa mila kutoka jamii ya wafugaji pia walipata nafasi ya kupaza sauti na kutaka serikali na jamii iheshimu maamuzi wanayoyatoa kama viongozi katika jamii.