F Jifunze kutengeneza chakula cha kuku mwenyewe | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Jifunze kutengeneza chakula cha kuku mwenyewe

Vyakula vya kuku vinaweza kupatikana madukani au kutengenezwa na mfugaji mwenyewe. Ili kuku aweze kukua haraka na kutoa mazao mengi na bora ni lazima chakula kitengenezwe katika mchanganyiko wenye uwiano mzuri uliopendekezwa. Chakula hicho lazima kiwe na viinilishe muhimu kama vile protini, wanga, madini na vitamini. Hakikisha chakula unachotengeneza kina mchanganyiko wa vyakula vifuatavyo:

 Vyakula vya kujenga mwili kama vile jamii ya kunde, samaki, dagaa, mashudu ya ufuta, pamba na alizeti.

 Vyakula vya kulinda na kukinga mwili usipate maradhi kama vile mafuta ya samaki na majani mabichi kama kabichi, michicha, majani ya mpapai na nyasi mbichi.

 Vyakula vinavyojenga mifupa kama vile aina ya madini, chokaa, mifupa iliyosagwa na chumvi. Ukosefu wa vitamini na madini kama Kalsiamu na Fosforasi husababisha matege, kukunjamana kwa vidole, kufyatuka kwa misuli ya goti na kupofuka macho.

Maji ni muhimu sana kwani husaidia kulainisha na kurahisisha usagaji wa chakula, na kupunguzajoto. Wakati wajoto kali kuku wapewe maji mengi.

Kabla ya Kutengeneza Chakula Lazima Mtengenezaji Ajue haya Yafuatayo:-

 Jinsi ya kupata vyakula vya aina mbali mbali.

 Kiasi cha viinilishe vinavyohitajika kwa kuzingatia umri na aina tofauti ya kuku; kwa mfano vifaranga wanahitaji protini asilimia 18 hadi 22, kuku wanaokua asilimia 17 hadi 19 na kuku wa mayai asimilia 15 hadi 17. Vile vile madini aina ya Kalsiamu kiasi cha asilimia tatu hadi nne kinahitajika kwa kuku wa mayai na asilimia moja kwa kuku wa nyama na vifaranga.

 Viwango vya uchanganyaji wa aina za vyakula mbali mbali: Ili mtengenezaji aweze kutengeneza chakula bora ni muhimu afuate kiwango cha uchanganyaji kilichopendekezwa Kiasi cha aina moja ya chakula kinapozidi kinaweza kuleta madhara.

Jedwali lifuatalo linaonyesha kiwango kinachotakiwa kwa baadhi ya vyakula.

Vyakula na Viwango Vinavyohitajika katika Asilimia 100

Aina ya ChakulaKiwango cha Uchanganyaji (%)
VyakulaVifarangaKuku wa NyamaKuku wa Mayai
Mahindi707070
Ulezi204040
Mtama203030
Mpunga407070
Ngano54040
Pumba za mahindi102020
Pumba za Mpunga102020
Pumba za Mtama102020
Pumba za Ngano51515
Mashudu ya nazi103040
Mashudu ya Pamba5105
Mashudu ya Alizeti102020
Mashudu ya Ufuta10105
Damu iliyokaushvva555
Mifupa iliyosagwa557.5
Dagaa1055
Lusina iliyosagwa
(Lucerne meal) Lukina555
(Lcuecana meal)2.555
Chokaa555
Chumvi0.50.50.5
Soya102020
 Kuhusu kiasi cha viinilishe kama protini, wanga, madini na vitamini vilivyomo kwenye aina za vyakula vitakavyochanganywa, Mfugaji anashauriwa amuone mtaalamu wa mifugo aliyekaribu naye aweze kumsaidia na kumpa ushauri zaidi.

 Mchanganyiko uwe na zaidi ya aina moja ya vyakula kwa mfano vyakula vya kujenga mwili vitokanavyo na wanyama na mimea.

Mifano ya kutengeneza kilo 100 za chakula cha kuku:-

 Mfano wa chakula cha vifaranga kuanzia siku ya kwanza hadi majuma manne.

VyakulaKiasi (Kg)
Mahindi30.00
Pumba za Mahindi20.00
Soya18.00
Mashudu ya Alizeti20.50
Dagaa5.00
Mifupa iliyosagwa4.00
Chumvi0.50
Vitamini2.00
 Jumla100.00
 Mfano wa chakula cha kukuzia kuanzia Juma la nne hadi la nane.
VyakulaKiasi (kg)
Mahindi45.00
Pumba za Mahindi20.00
Mashudu ya pamba5.00
Soya20.00
Dagaa2.50
Mifupa iliyosagwa5.00
Chumvi0.50
Vitamini2.00
 Jumla100.00
 Mfano wa chahula cha kuku wa mayai kuanzia Juma la nane hndi la ishirini.
(a)(b)
VyakulaKiasi (Kg)VyakulaKiasi (Kg)
Mahindi45.00Mahindi45.00
Pumba za mahindi25.00Pumba za mahindi30.00
Soya5.00Soya5.00
MashuduyaAlizeti10.00Mashudu ya pamba5.00
Dagaa4.00Dagaa iliyokaushwa4.00
Damu3.00Mifupa iliyosagwa2.50
Chokaa3.00Chokaa3.00
Chumvi0.50Chumvi0.50
Vitamini2.00Vitamini2.00
 Jumla100.00100.00
 Mfano chakula cha kuku wa Mayai kuanzia Juma la lshirini na kuendelea:
(a)(b)
VvakulaKiasi (Kg)VvakulaKiasi (kg)
Mahindi50.00Mahindi40.00
Pumba za mahindi15.00Pumba za mahindi25.00
Mashudu ya Pamba5.00Mtama5.00
Soya18.00Mashudu ya Alizeti10.00
Dagaa4.50Dagaa4.00
Mifupa iliyosagwa3.00Damu ilyosagwa5.00
Chokaa2.00Mifupa iliyosagwa4.50
Chumvi0.50Chokaa4.00
Vitamini2.00Chumvi0.50
 Jumla100.00Vitamini2.00
 Jumla100.00