Kuna mambo ambayo unaweza kuyafanya na yakawa msaada kwako kwa wewe mwenye tatizo hili, njia hizo ni kama ifuatavyo.
1. Ukigundua unatatizo hilo, hakikisha unasafisha miguu yako mara kwa mara na kuikausha vizuri kabisa ili kuepusha unyevunyevu.
2. kila unapovaa viatu vya kufunika hakikisha unavaa soksi safi na safi.
3. Epuka kurudia soksi kabla ya kufua au ambazo hazijakauka vizuri kwani huweza kuchangia miguu kunuka zaidi.
4. Usivae viatu vilivyoloa na endapo ikatokea umenyeshewa, hakikisha unavianika kwenye hewa ili vikauke ili kupunguza uwezekano wa kutoa harufu.
Hata hivyo licha ya kuwepo kwa sababu mbalimbali zinazochangia tatizo hili la kunuka miguu, ukweli utabaki kuwa uchafu ndio chanzo kikuu cha miguu kutoa harufu.
Endapo utahisi tatizo ni kubwa zaidi basi unaweza kuwaona wataalam ili kupata ushauri na tiba zaidi.