Kenya kuteketeza tani 100 za meno ya Tembo

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta leo ameongoza zoezi la kuteketeza shehena kubwa ya meno ya Ndovu zaidi ya tani 100 katika hatua ya kuonyesha dhamira ya kuokoa idadi ya Tembo barani Afrika.

Rais Kenyatta ameongoza zoezi hilo la kuchoma meno hayo ya Ndovu katika viwanja vya Nairobi National Park, na moto huo utadumu kwa siku kadhaa,idadi ya meno hayo yanayochomwa ni sawa na Tembo 6,700 na tukio hilo ni kubwa kwa historia ya kuchoma Meno ya Tembo.

Marufuku ya biashara ya Meno ya Tembo ilitolewa na viongozi wa Afrika na rais Kenyatta ambaye ni mwenyeji wa Mkutano wa Kimataifa utakaojadili masuala ya kupinga biashara ya Meno ya Tembo utakaofanyika huko Nanyuki,Rais Kenyatta alikaririwa jana akisema kwamba kuuwawa kwa Tembo ni kuuwawa kwa utalii barani Afrika.

Baadhi ya wanaharakati wa wanyama wamesema kuchoma kiasi kikubwa kama hicho kikiwa adimu kunawewza kuongeza dhamani ya na kuchochea uwindaji haramu wa wanyama hao.

Botswana ambayo ina idadi kubwa ya Tembo takribani nusu ya Tembo wote barani Afrika wanaokadiriwa kufikia zaidi ya laki nne imepinga zoezi hilo na rais wa nchi hiyo hatahudhuria zoezi hilo la Nairobi katika viwanja vya National Park.