Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya kikao cha dharura baada ya kiongozi wa waasi nchini Sudan Kusini Riek Machar kushindwa urejea Juba, kama sehemu ya mkataba wa amani.
Kikao hicho kiliitishwa na Marekani baada ya Bwana Machar kushindwa kwa mara ya pili kurejea nchini Sudan kusini na hivyo kuyapunguza matumaini ya kupiga hatua ya kuvimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo dumu kwa miaka miwili.
Kulingana na makubaliano hayo, kiongozi huyo wa waasi alipaswa kujiunga na Rais Salva Kirr katika serikali mpya ya mpito ya muda wa miezi 30 hadi uchaguzi utakapofanyika.
Akizungumza na Kituo cha Al jazeera live Machar mwenyewe amesema kuwa ameshindwa kurejea mjini Juba kutokana na ndege aliyotarajia kusafiria kukosa kibali cha kutua katika anga ya Sudan ya kusini.
Machar alitarajiwa kurejea nchini Sudan Kusini tangu siku ya jumatatu kuchukua wadhifa wake wa zamani wa makamu wa kwanza wa rais ambapo kiongozi huyo alitoroka mjini Juba mwaka wa 2013 baada ya rais wa nchi hiyo Salva Kirr kumtuhumu kuongoza jaribio la mapinduzi ya serikali yake.