Ajenda ya UKAWA yatekelezwa kwa vitendo bungeni.

Ajenda ya kambi ya upinzani Bungeni kutokuwa na imani na naibu spika wa Bunge Tulia Ackson Mwasasu imeanza kutekelezwa kwa vitendo baada ya wabunge wa upinzani kutoka nje baada ya Naibu Spika kuanza kuongoza kikao cha bunge na wabunge hao kutoka nje.

Wabunge wa upinzani wametoka nje asubuhi mara baada ya kuanza kwa kikao cha leo ambapo wamesubiri baada ya Naibu Spika kusoma dua ya kuliombea bunge wabunge wote wa upinzani wamenyanyuka na kutoka nje.

Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe amesema kwamba wabunge wa upinzani hawatashiriki vikao vya Bunge siku akiongoza Naibu Spika Tulia Ackson kwa sababu hawana imani naye namna anavyoendesha vikao vya bunge na kusimamia sheria na taratibu za bunge.

''Tatizo kubwa la Bunge la 11 ni Naibu Spika, Bunge linavurugika na maamuzi ya bunge yanapuuzwa ni baada kuja kwa huyu mtu anayeitwa Tulia Ackson'' Amesema Mbowe
Vile vile Mbowe amesema kwamba kama serikali itaona Naibu Spika ni wathamani kuliko wananchi ambao wanataka kusikiliza hoja za wapinzani basi upinzani utafanya siasa sehemu nyingine .

Aidha Naibu Spika wa Bunge amewataka wananchi kuelewa kwamba kilichofanya wabunge kusimamishwa siyo hoja ya wanafunzi wa UDOM bali ni wabunge hao kutotii sheria na kanuni za bunge na kusababisha fujo bungeni Januari 27, 2016 kwa kushinikiza kiti kiruhusu kujadiliwa kwa hoja ya bunge kurushwa live jambo ambalo lilikuwa limekwisha tolewa maamuzi.