FastJet walalamikiwa na wateja wao wanaotumia Mtandao kwa malipo

Baadhi ya Abiria wanaosafiri kwa kutumia kampuni ya Ndege ya Fast jet ya jijini dsm ambao wanatumia mtandao kulipia huduma ya Usafiri au mizigo wamelalamikia kuwapo kwa Usumbufu kunakodaiwa kunatokana na mtandao na kulazimika kulipia gharama ya mizigo mara mbili kwa madai kuwa huduma hiyo inachelewesha kuleta majibu kwa sababu ambazo hazijafamika.

Wakizungumza katika ofisi za Fastjet zilizopo tazara jijini Dsm abiria hao ambao wameshindwa kupata Ufumbuzi wa madai yao kwa kutakiwa kuwasiliana na uongozi kwa njia ya mtandao wamedai kuwa wameendelea kupata Usumbufu usio wa lazima huku wakidai kuwa hawataondoka eneo hilo mpaka madai yao yafanyiwe kazi.

Chanel ilitaka ufafanuzi kuhusu madai hayo afisa aliyekuwapo katika ofisi hizo alidai kuwa hawezi kuzungumza chochote huku pia akikataa kutoa Ushirikiano kwa idara zinazohusika ili kupata ufafanuzi wa madai hayo.