Maombi ya watumiaji wa Kivuko cha Kigamboni

Wananchi  wanaotumia kivuko cha Kigamboni jijini Dar es salaam wameiomba serikali kuongeza kivuko kipya ili kupunguza adha ya usafiri  inayowakabili kufuatia kuharibika kivuko kimoja kwa muda mrefu, hali  inayosababisha kero kubwa kwa watumiaji wa kivuko hicho nyakati za asubuhi na jioni

Wakizungumza na Channel Ten  wananchi hao wamesema kivuko kilichobaki cha MV Kigamboni na MV Hadija ni vidogo na haviwezi kumudu kubeba abiria pamoja na magari, jambo ambalo linahatarisha maisha ya wananchi wanaotumia usafiri huo.

Katika kukabiliana na adha hiyo wameiomba serikali japo kupunguza gharama zinazotozwa kwenye daraja la Nyerere ili kutoa fursa kwa magari mengi zaidi kutumia daraja hilo huku wananchi wakibakia kwenye kivuko.

Wananchi hao wamedai kuwa sasa ni zaidi ya mwezi mmoja wamekuwa wakikumbana na adha hiyo baada ya kivuko cha Mv magogoni na kusitisha safari zake kwa ajili ya matengenezo.