Mauaji Kiteto sasa Basi wazee wala Kiapo mbele ya Viongozi wa Serikali

Wazee kutoka jamii ya wafugaji na wakulima wilayani Kiteto mkoani Manyara wameazimia kula kiapo mbele ya viongozi wa  Serikali katika eneo la Embolei Mutangusi ambalo limekumbwa na mgogoro wa muda mrefu baina ya wakulima na wafugaji ambao husababisha vifo na uharibifu wa mali.

Wazee hao wameiambia Chamnel Ten kuwa wameamua kufikia hatua ya hiyo ya kiapo huku wakitaraji kufanya hivyo mbele ya viongozi wa juu wa serikali kutokana na kuchoshwa na mapigano ya wafugaji na wakulima inayosababisha wao kupoteza ndugu na jamaa zao.

Nao viongozi wa dini wilayani hapa wamepata fursa yakueleza namna ambavyo mgogoro huo wa aridhi umeadhiri.

Aidha kutokana na zoezi la kuapa katika eneo hilo kuoenekana kuwa na nguvu zaidi kwa upande mmoja mkuu wa mkoa wa manyara dkt joel bendera ameagiza pande zote kukutana na kuridhia hatua hiyo pamoja na kutoa nafasi kwa viongozi wa serikali ngazi ya taifa kuhudhuria  katika tukio hilo linalotarajiwa kufanyika hivi karibuni.