Tuzo ya Rais kwa Wazalishaji Bora na kutoa kauli hii kwa Mawaziri

Rais Dk.John Pombe Magufuli ameahidi kumfuta kazi mara moja Waziri au Katibu Mkuu yeyote  anayehusika na uwekezaji nchini iwapo itathibitika amekwamisha kwa namna yoyote ile ikiwamo rushwa, juhudi zake za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2015.

Dk. Magufuli ametoa angalizo hilo jijini Dar es salaam katika hafla ya tuzo ya Rais ya uzalishaji bora na viwanda kwa mwaka 2015, ambapo pia ametoa wito kwa wazalendo kujitokeza zaidi na kuwekeza kwa kuwa serikali yake imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa nchi viwanda.

Akijibu changamoto zinazowakabili wawekezaji na wenye viwanda, Dk. Magufuli amesema anafahamu hizo ikiwemo vikwazo kutoka watendaji wa Serikali wasio waaminifu,urasimu, rushwa na kodi alizoziita za hovyo hovyo.

Katika hatua nyingine, Dk, Magufuli amewataka wawekezaji na wenye viwanda kupuuza madai yanayoenezwa na watu wasio na nia ya njema kuwa anawachukia matajiri na wafanyabiashara,ambapo amesisitiza hawezi kuiongoza nchi bila wao,ingawa ameweka bayan kwaamba hawezi kamwe kuwachekea wale wanaokwepa kodi.

Kampuni ya Bia Tanzania ndiyo iliyoibuka mshindi wa jumla katika tuzo ya Rais ya uzalishaji bora na viwanda kwa mwaka 2015.