Wamisri kuwasili kesho, kuvaana na Stars Jumamosi

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Misri kinatarajiwa kuwasili hapo kesho kwa ajili ya mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars wa kuwania fainali za AFCON utakaopigwa jumamosi ya Juni 04 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF, Alfredy Lucas amesema, mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Gabon huku taratibu zote kuhusu mchezo huo zikiwa zimekamilika.

Katika mchezo wa awali uliochezwa nchini Misri hapo mwaka jana, Taifa Stars ilipoteza mchezo huo baada ya kuchapwa mabao 3-0.

Baada ya mchezo dhidi ya Misri, Stars itacheza mechi ya mwisho na Nigeria Mjini Lagos Septemba mwaka huu.