Aliyembaka bintiye atupwa jela miaka 30

Rombo. Mahakama ya Wilaya Rombo mkoani Kilimanjaro, imemuhukumu adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela  mkazi wa wilayani humo, Japhet Temba (30) baada ya  kukutwa na hatia ya kumbaka mtoto wake mwenye umri wa miaka 15.

Akitoa hukumu hiyo leo, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakam hiyo, Naomi Mwerinde amesema kutokana na kosa hilo, mahakama yake imejiridhisha na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka bila kutia shaka yoyote.

Awali, ilidaiwa mshitakiwa alitenda kosa hilo eneo la Holili, Kata  ya Mengwe wilayani Rombo huku  akijua kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.