Dogo mfaume akiri kutumia madawa ya kulevya




 Rehema Chalamila maarufu kama Ray C aliwahi kutangaza hadharani juu ya maamuzi yake ya kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya ingawa kinachoendelea kuonekana hivi sasa kupitia mitandao ya kijamii hakiendani na yale aliyoyasema na badala yake anaonekana kuendelea kubwia unga.

Baada ya kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya kwa takriban mwaka mmoja na nusu Juni 22, mwaka huu rapper wa ngoma ya #fununu aliamua kujitokeza mbele ya wanahabari kukiri kwamba alikuwa mtumiaji mzuri wa madawa hayo licha ya kutumia nguvu kubwa kukanusha tetesi hizo kipindi cha nyuma.


 Young D ambaye aliamua kuachana na madawa hayo kwa kufuata nyayo za Chid Benz alifikia maamuzi hayo baada ya kuona anapotea, licha ya kumdis Babu Tale ambaye alichukua uamuzi wa kumsaidia Chid kwenda ‘rehab’ ambaye hivi sasa amerejea katika hali yake ya kawaida kwa kipindi kifupi.

Baada ya rapper hawa kuonesha hadharani msimamo wao thabiti juu ya kuachana na utumiaji wa dawa za kulevya, safari hii mkali wa ngoma ya #kazi ya dukani maarufu kama Dogo Mfaume ameamua kujifichua kama mmoja wa waathirika wa madawa hayo na kuamua kuachana nayo.