Hakuna polisi wanaopiga raia Pemba- Masauni

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Masauni amesema kwamba hakuna ukweli kwamba katika kisiwa cha Pemba kuna askari polisi wanapiga raia bali habari hizo ni zauongo na za kupuuzwa.

Masauni ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la viti maalumu (CCM) aliyetaka kujua ukweli wa tarifa zinazotoka kisiwa cha pemba zinazosema kwamba askari polisi wanapiga raia bila hatia.

Naibu Waziri Masauni akijubu swali hilo amesema kuwa askari polisi kote duniani wanafanaya kazi kwa mujibu wa sheria na hakuna kitendo cha askari kupiga raia bali kuna vitendo vinafanywa na vyama vya siasa ili kulipaka tope jeshi la polisi.

Wanaolalamikani watu wanaofanya usanii na maigizo na kulidhalilisha jeshi la polisi na kuwataka askari polisi kuendelea na kazi yao ya kulinda amani ya nchi.