Kauli ya Asha Baraka imenichoma- Ali Choki

Mapema siku chache zilizopita Mmiliki wa Twanga pepeta Asha Baraka aliongea na Enewz na kutufahamisha kwa sasa amechoshwa na maswala ya kutangaza wasanii wanapoingia kwenye band yake

Hata hivyo Asha Baraka ameendelea kusema kitendo cha wasanii wa band kutokana na kubadili band imekuwa hali ya kawaida na kuona ni kama utoto wasanii wanakimbia wakirudi wanataka waitiwe waandishi wa habari kwa ajili ya kutangazwa YEYE HATA ITA WASANII TENA.

Kauli hiyo imemchoma sana msanii mkongwe wa muziki wa dance Ali Choki na kusema kuwa mama anakosea sana kwa sababu wao tayari ni wasanii hivyo kitendo cha kuingia kwenye band kimya kimya bila press comference ni kuwashusha kimziki.

Choki amewasisitiza wasanii wenzake wa dansi kuimba vitu vipya na kuuendeleza mziki wa dansi kama ilivyokuwa enzi zake yeye na kina Mwijuma Muumini,hakusita pia kuwaomba wadau wa muziki kuendelea kuusapoti mziki wa dansi,huku akisema anatarajia kufanya sherehe ya kutimia miaka 30 yake katika mziki wa dansi.