‘Koboeni mahindi kuondoa sumu’

Dar es Salaam. Shirika lisilo la kiserikali la World Vision limesema kuna umuhimu wa kukoboa mahindi ili kuondoa sumu zenye athari kwa binadamu.

Akizungumza katika mkutano wa wazalishaji hao jana, meneja mradi wa urutubishaji vyakula wa World Vision, Symphrose Uisso alisema: “Kwanza uhifadhi wa mahindi katika nchi yetu uko duni sana. Matokeo yake mahindi huota sumu ambayo ni hatari kwa afya ya binadamu kwani inaweza kusababisha saratani. Vilevile viuatilifu vinavyotumika kuzalisha na kuhifadhia nafaka vina madhara.“Baada ya kukoboa mahindi tunayo teknolojia ya kuongeza virutubisho vinavyokosekana kwenye unga wa mahindi,” alisema.

Shirika hilo pia linakamilisha mchakato wa kuwafadhili wazalishaji na wasambazaji wa unga wa mahindi jijini Dar es Salaam mashine za kuongeza virutubisho.