KUFUATIA UINGEREZA KUJITOA UMOJA WA ULAYA, TIMU NYINGI ZAPATA KWIKWI KWENYE SWALA LA USAJILI WA WACHEZAJI

 Timu nyingi zinazoshiriki kwenye ligi kuu nchini Uingereza zimekumbwa na kigugumizi cha kufanya usajili katika kipindi hiki ambacho nchi yao imejitoa katika umoja wa ulaya (EU).

Wakili wa masuala ya michezo, Carol Couse amedai kuwa uamuzi huo tayari umeanza kuleta athali ambapo sarafu ya nchi hiyo imeporomoka na kuzidiwa na sarafu ya Euro, hivyo basi vilabu vyote 20 vya ligi hiyo ambavyo vilikuwa vinapiga kampeni Uingereza isijitoe kwenye umoja huo, kwa kuwa na wasi wasi wa kupanda kwa gharama za vibali vya kufanyia kazi kwa wachezaji wa kigeni watakao sajiliwa.

Msimu mpya wa usajili ulifunguliwa majuma mawili yaliopita, lakini kuna wasi wasi timu nyingi hasa zile zisizo kuwa na uwezo mkubwa kifedha itabidi zisubiri hadi hali ya sarafu hiyo (POUND) itulie ndipo waendelee na mchakato wa usajili.

Carol Couse ambaye hufanya kazi na timu kadhaa kubwa ikiwemo Manchester United amebainisha kuwa hali hiyo itavilazimu baadhi ya vilabu kufanya usajili wa haraka haraka ili kukimbizana na muda kwani haijulikani hali ya thamani ya sarafu hiyo itachukuwa muda gani kurudi kwenye hali yake ya kawaida.

Baadhi ya vilabu ambavyo vimeisha fanya usajili uliokamilika mpaka sasa ni Liverpool waliosajili wachezaji 3 ambao ni kipa wa kimataifa wa Ujerumani Loris Karius, Mlinzi wa kimataifa wa kameruni Joel Matip na Mshambulizi wa kimataifa wa Senegali Sadio Mane. Tottenham wamemsajili Victor Wanyama na Chelsea wamemsajili Mitchy Batshuayi.