BREAKING NEWS: LOWASSA ATOFAUTIANA NA CHADEMA,AMPA BIG UP RAIS MAGUFULI

KWA mara ya kwanza,mara baada ya uchaguzi mkuu kuisha mwaka jana ,Aliyekuwa Mgombea Urais wa CHADEMA,Edward Lowassa leo hii amefunguka na kukiri juu ya uwezo wa JPM katika kutenda kazi.

Lowassa ambaye leo asubuhi alikuwa katika mahojiano katika chombo kimoja cha Luninga,alisikika akimsifia Dr Magufuli huku akidai kuwa kama angelikuwa ni yeye ndio Rais angefanya zaidi ya JPM.

Hii inakuwa ni sawa na kwenda kinyume na Chama chake ambapo mara kadhaa wamekuwa wakiuponda utawala wa Rais Magufuli huku wengine wakimuita dikteta

 Follow
 Jamii Forums @JamiiForums
Lowassa: Rais Magufuli anafanya vizuri ila mimi ningefanya vizuri zaidi, badala ya kuanza na madawati ningeanza na maslahi ya walimu #JFLeo
10:17 AM - 31 Jul 2016
  57 57 Retweets   85 85 likes