DRC: Upinzani wamtaka Kabila aachie madaraka

Makumi ya maelfu ya wafuasi wa upinzani wamekusanyika mjini Kinshasa, Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, kupinga uwezekano kuwa uchaguzi wa rais huenda ukaahirishwa.

Makumi ya maelfu ya wafuasi wa upinzani wamekusanyika mjini Kinshasa, Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, kupinga uwezekano kuwa uchaguzi wa rais huenda ukaahirishwa.

Upinzani unaona kuna jaribio la kuahirisha uchaguzi, ili kumruhusu rais Joseph Kabila abakie madarakani.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanywa Novemba, lakini tume ya uchaguzi, imesema inaweza kuchukua miezi 16, kurekibisha orodha za wapigaji kura.

Upinzani unaona kuna jaribio la kuahirisha uchaguzi, ili kumruhusu rais Joseph Kabila abakie madarakani.
Rais Kabila amehudumu kwa mihula miwili kwa hivyo haruhusiwi kikatiba kuwania uchaguzi ujao
Kufuatana na katiba ya nchi hiyo kubwa ya Afrika , Rais Kabila anatakiwa kuondoka madarakani mwaka huu, baada ya kutumika kwa mihula miwili.

Hata hivyo mahakama ya kikatiba nchini humo yameamua abakie madarakani, hadi uchaguzi utapofanywa.