Seli ya kifahari yapatikana gerezani Paraguay

Seli ya kifahari gerezani yapatikana Paraguay
Polisi nchini Paraguay wamegundua seli ya kifahari katika gereza la wafungwa sugu nchini humo Tacumbu.

Seli hiyo ilikuwa ya mfungwa mmoja ambaye ni kiongozi wa genge la ulanguzi wa mihadarati.
Katika seli hiyo ya kipekee yenye vyumba vitatu polisi waligundua mlikuwa na sebule ,maktaba, jikoni, na chumba cha kutizama televisheni.

Mlanguzi wa mihadarati raia wa Brazil Jarvis Chimenes Pavao ndiye aliyekuwa akiishi humo
Mlanguzi wa mihadarati raia wa Brazil Jarvis Chimenes Pavao ndiye aliyekuwa akiishi humo na mfungwa yeyote aliyetaka kuishi naye humo alitozwa kodi ya dola elfu tano pesa taslim.
Lakini kwanini waishi humo ?

Seli ilikuwa na vyumba vitatu hata na jikoni
Mlikuwa na viti vya kifahari, yaani mwenyeji angeweza hata kutazama vipindi ya runinga, video , angeweza kuoga maji ya moto .
Kuta yake ilikuwa imewekwa matofali ya kisasa na ya kuvutia.
Uchunguzi umeanza kubaini ni maafisa wagani katika gereza hilo waliomruhusu mlanguzi huyo wa mihadarati kuishi maisha hayo ya kifahari humo gerezani.

Bwana huyo alikuwa akiigiza maisha ya mlanguzi hodari wa mihadaratii kutoka Colombia Pablo Escobar.
Sadfa ni kuwa mle ndani mlikuwa na video moja iliyokuwa na simulizi ya maisha ya mlanguzi hodari wa mihadarati kutoka Colombia Pablo Escobar.

Escobar ambaye aliuawa mwaka wa 1993 alikubaliana na viongozi wa idara ya magereza nchini Colombia kuwa atakubali kutumikia kifungo chake gerezani ilimradi tu aruhusiwe kuijenga seli atakamoishi.

Wafungwa wenzake wamehuzunishwa na ugunduzi huo wa polisi ambao wanadai umewapokonya bwana mkarimu sana humo gerezani.

Mfungwa tajiri mlanguzi wa madawa ya kulevya aliishi humo
Mmoja wa wafungwe wenza bwana Antonio Gonzalez amenukuliwa akisema kuwa alikuwa maarufu sana ,na aliwapenda wote aliokutana na kujumuika naye.
''Alikuwa bwana mcheshi sana ''
Mfungwa huyo tajiri wa kupindukia amehamishwa hadi katika gereza lililoko karibu na mji mkuu wa Asuncion.
Mlikuwa hata na maktaba ya video
Polisi waligundua seli hiyo ya kipekee katika gereza hilo la Tacumbu baada ya kudokezewa kuwa kulikuwa na mtu aliyeagiza aletewe bomu mle ndani.
Yamkini rais huyo wa Brazil Chimenes Pavao ambaye alikuwa anatarajiwa kukamilisha kifungo chake cha miaka minane gerezani hapo mwakani hakutaka arejeshwe Brazil, kwa hivyo alikuwa amepanga njama aletewe bomu ambalo angelitumia kulipua ukuta wa gereza hilo na kutoroka.