Unyanyasaji wa wanawake na watoto jamii ndio tatizo na sio sheria.

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungnao Dr Tulia Ackson Mwansasu amesema hata zikiwepo sheria kali dhidi ya wanaonyanyasa wanawake na watoto bado wahalifu hao watendelea kuwepo kutokana na jamii bado kuwa mbali kufahamu umuhimu wa tatizo hilo

Dr Tulia ametoa msimamo hapa Zanzibar huo wakati akitoa maoni yake baada ya kuzindua taasisi isiyo ya serikali ya rafiki wa wanawake na watoto hafla ambayo ilifanyika zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo mawaziri,wabunge na wawakilishi ambapo amesema sheria peke yake haisadii lakini jamii ndio inapaswa  kuelimishwa na kubadilika ingawa amesema serikali za Tanzania zinachukua juhudi kuweka sheria mbalimbali za kudhibiti.

Mapema mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya rafiki wa wanawake na watoto Mhe Tauhida Gallos Nyimbo amesema lengo lao kubwa la kuunda taasisi hiyo ni kuwafikia akina mama na watoto ambao wanashindwa kupata haki zao na wanapata mateso lakini hawana msaada wowote kutoka kwa jamii.

Katika hafla hiyo Naibu Spika wa Bunge Dr Tulia Ackson aliweza kuendesha na kusimamia harambee ambapo jumla ya shilingi milioni 17 zilipatikana kupitia mnada na ahadi na fedha taslimu huku taasisi hiyo ikiwa ni yakwanza kuanzishwa Zanzibar yenye lengo la kwenda moja kwa moja kwa watu wa kipato cha chini.