Waislamu wajiunga na wakatoliki katika ibada

Waislamu wajiunga na wakatoliki katika ibada
WaIslamu zaidi ya mia moja wamejumuka na Wakatoliki katika sala iliyohudhuriwa na waumini wengi katika Kanisa moja huko Rouen, Ufaransa.
Tukio hilo limewadia , siku tano baada ya kasisi wa kanisa hilo , kuuawa na wapiganaji wa Kiislamu.

Muungano huo unalenga kuonesha umoja dhidi ya mauaji ya kasisi
Makanisa sehemu mbali mbali za Ufaransa, yaliwaalika WaIslamu wajumike nao kwenye maombi leo, kuonesha wanakanusha mauaji hayo.
Mauaji ya hivi karibu kabisa yaliyotekelezwa na wapiganaji wa Kiislamu, yameshtua Ufaransa.

Kasisi huyo wa umri wa miaka 86, Kasisi Jacques Hamel, aliuwawa akiwa kwenye maombi.