Askofu aliyenaswa akifanya mapenzi na mkwe wake ajitetea

Askofu aliyenaswa akishiriki mapenzi na binamu wa mkewe amekana madai

–Askofu Jonathan Musyoki Muthoka wa Jesus Liberation Ministry anadai mkewe anaeneza uvumi huo ili kumharibia kanisa

Askofu Jonathan Musyoki Muthoka aliyenaswa akishiriki mapenzi na binamu wa mkewe amekana madai hayo.

Irene Kavata aliweka kamera za CCTV nyumbani kwao zilizomnasa mumewe akishiriki mapenzi na binamu yake ambaye alikuwa amemuajiri kama mjakazi wa nyumbani.

Lakini Askofu Muthoka wa kanisa la Jesus Liberation Ministry amekana vikali madai hayo.

“Hata siwezi kulala naye kwa sababu ya uhusiano tulionao. Je, itakuwaje nifanye kitendo kama hicho nyumbani kwa mke wangu?” alisema.

Badala yake, Askofu Muthoka anamshutumu mkewe kwa kupanga njama ya kuniharibia sifa na kisha kunivunjia kanisa. Asema tabia za mkewe zimemletea presha na kuwaathiri watoto.

“Ameajiri wajakazi zaidi ya 70 tangu tufunge ndoa 2008 kwa sababu ananishuku bila sababu zozote. Mbona alimtaja tu huyo mwanadada na si mwingine yeyote,” aliambia The Nairobian.

Askofu Muthoka alisema lengo la mkewe ni kumfyonza pesa na kuharibu familia yao.

Anadai mkewe siku zote amekuwa na tashwishi zisizo za kimsingi eti kwa sababu askofu husafiri sana.

“Mimi husafiri sana. Wakati mmoja nilikuwa nimeenda kwa mkutano wa injili Mombasa lakini akadai eti nimeenda kufanya mambo mengine,” akaongeza.

Kavata anasemekana kupanda mori alipogundua mumewe alikuwa ametengana naye kwa muda wa mwezi mmoja na kusema kuwa ameenda mahakamani kusaka malipo ya utunzi na malezi ya watoto.

Kavata aliiambia mahakama kuwa mumewe huyo askofu amekuwa na mipango ya kando tangu 2008 walipofunga ndoa ya kifahari.