Chege: Warembo wa video za muziki Bongo wanazingua

Msanii wa muziki kutoka TMK Wanaume Family, Chege amefafanua kuwa sababu inayowafanya wasanii washindwe kuwatumia warembo wa video za muziki wa ndani kwenye video wanazoenda kushoot nje, ni kutokana na kutokuwa serious.

Chege ambaye wimbo wake ‘Waache Waoane’ akiwa na Diamond unafanya vizuri kwenye TV na redio, ameiambia East Africa TV, kupitia kipindi cha Planet Bongo cha wiki iliyopita kuwa alitaka kuwachukuwa warembo watano wa hapa Bongo kwenda Afrika Kusini kushoot nao video yake hiyo mpya.

“Nilitaka kuondoka na models watano, lakini kati ya hao mmoja tu ndiye alikuwa na passport na hawa wengine hawakuwa nazo. Sidhani kama kweli walikuwa hawana lakini ni kama walikuwa wanazingua,” amesema Chege.

Msanii huyo ameongeza kuwa warembo wa nje hawasumbui kwakuwa hata ukiwataka 15 ukipiga simu baada ya muda unatumiwa picha za warembo 50 uchague unaowataka kuwatumia kwenye video yako.