FAHAMU CHANZO CHA UZITO MDOGO AU WEMBAMBA SANA NA MATIBABU YAKE

japokua dunia ya sasa inakabiliwa na tatizo kubwa la watu kua wanene sana lakini kuna changamoto ya watu ambao ni wembamba sana kiasi kwamba wembamba wao ni hatari kiafya. tafiti zinaonyesha kwamba ukiwa mwembamba sana una hatari ya kufa mapema kwa 100% lakini ukiwa mnene sana una hatari ya kufa mapema kwa 50% hivyo unaweza kuona kwamba wembamba sana ni hatari kuliko unene sana.

Uzito mdogo maana yake nini? 
kua chini ya 18.5 kwa vipimo vya body mass index ambavyo vinapatikana kwa kuchukua uzito wako kwa kilogram na kugawanya kwa [ urefu wako zidisha mara mbili kwa kipimo cha mita]. mfano una kilo 75 urefu wa 1.75m unachukua 75 gawanya kwa[1.75x1.75] jibu ni 24.4 huyu yuko kwenye uzito sahihi. lakini  ukizidi body mass index ya 25 umezidi unene na chini ya 18 umezidi wembamba.
tatizo la kua na uzito mdogo linawaathiri wanawake zaidi na huwatesa sana kisaikolojia kwani wengi wao hutamani kua na miili mzuri kama wenzao.

Chanzo ni nini?
kuna sababu mbalimbali zinaweza kuchangia mtu kua na uzito mdogo au mwembamba sana kama ifuatavyo.

Matatizo ya kushindwa kula; tatizo la kutokua na hamu ya kula, hofu ya kunenepa sana iwapo utakula sana hii inawasumbua sana wasichana wanaopenda mambo ya urembo, matatizo ya kisaikolojia huchangia sana mtu kua mwembamba kitaalamu tunaita anorexia nervosa.

Matatizo ya mfumo wa homoni; kuna ugonjwa unaitwa hyperthroidism, huu ni ugonjwa ambao unafanya mwili kufanya mambo yake kwa haraka sana huanza na dalili za kuharisha, kula sana, kutokwa sana jasho, kusikia joto sana na kadhalika. halii hii hupunguza uzito sana na mtu hawezi kuongezeka uzito bila kutibiwa ugonjwa huu.

Magonjwa ya utumbo wa chakula; kuna magonjwa ya utumbo yanayoweza kusababisha mtu kushindwa kula aina fulani ya vyakula au kuharisha kila anapokucha chakula fulani. hii hupunguza sana uzito mfano tropical sprue.

Ugonjwa wa kisukari; kua na ugonjwa wa kisukari ambayo haitibiwi vizuri humaliza hifadhi yote ya vyakula mwilini na kufanya watu wawe wembamba sana.

Kurithi; kuna baadhi ya koo watu ni wembamba tu kwanzia bibi mpaka wajukuu, japokua wembamba huu sio hatari lakini ukiwa chini ya vipimo nilivyotaja basi ni hatari.

Ugonjwa wa saratani; magonjwa yote ya saratani hutumia kiasi kikubwa cha chakula na kumfanya mtu apungue uzito sana.

Baadhi ya magonjwa ya kuambukizwa; magonjwa kama ukimwi na kifua kikuu huudhoofisha mwili sana na kumuacha na uzito mdogo sana.

nini madhara ya uzito mdogo?
uzito mdogo husababisha magonjwa ya akili, kushusha kinga ya mwili na kuugua mara kwa mara, kukosa hedhi, ugumba, kuwa na mifupa milaini inayovunjika kirahisi na kadhalika.

kitu gani ufanye kuengezeka uzito?
kimsingi kanuni ya kuongezeak uzito ni ndogo ya kula sana kuliko kazi unazofanya, unaweza kunywa soda nyingi, sukari nyingi, na vyakula vyovyote vya haraka[fast foods] lakini hio sio njia nzuri ya kuongeza uzito kwani vyakula hivyo huambatana na magonjwa hatari ya mwili kama kisukari na magonjwa ya moyo lakini pia unaweza ukapata unene mbaya. njia nzuri ni kufuata yafuatayo.

Kula vyakula vingi; changanya vyakula vya aina mbalimbali na ule angalau mara tatu kwa siku na ushibe. vyakula vya protini kama nyama, mayai, samaki, maziwa, karanga na kadhalika, vyakula vya wanga kama ugali,wali, viazi,mihogo, na kadhalika, vyakula vya mafuta kama mafuta ya siagi, alizeti,korie na kadhalika. jitahidi ule mara tatu au mara nne ya chakula unachokila sasa hivi.
protini ni muhimu sana kwani yenyewe ndio inayojenga misuli ya mwili hivyo ni vizuri kula kwa wingi.

Fanya mazoezi ya kubeba chuma; nenda gym uanze mazoezi ya kubeba chuma kwani mazoezi haya yatazuia kuongezeka uzito kwa mafuta na kukupa ongezeko la uzito la misuli na kua na mwili mzuri. mazoezi ya chuma ni kwa jinsia zote.

Tibu ugonjwa kama upo; kama unahisi kuna ugonjwa wowote unaokusumbua hakikisha umetibiwa na kupona au unapata matibabu yake hata kama hautibiki kabisa basi angalau tumia dawa za kupoza mfano kisukari au ukimwi, usipotibu chanzo cha ugonjwa unao kupunguza uzito huweza nenepa kwa njia yeyote ile.

Usinywe maji kabla ya kula; tabia hii itakufanya ujaze tumbo na maji na kukufanyaushindwe kula chakula cha kutosha.

Kula mara kwa mara; usijibanie kula kabisa, kila ukipata nafasi we kula tu, ikibidi kula hata muda wa kwenda kulala kwani inasaidia sana kuongezeka uzito.

Kunywa maziwa mengi; ukipata kiu ya maji kunywa maziwa kwanza kama yapo afu ndio unywe maji kwani maziwa yana protini muhimu kwa ajili ya kuongeza uzito.

Jaribu virutubisho maalumu kwa ajili ya kuongeza uzito; kuna virutubisho vingi vimetengezwa maalumu kwa ajili ya kazi hii, ambavyo vinauzwa na kampuni mbalimbali. vitutubisho hivi vinakuwa na protini na madini mengi kuliko chakula cha kawaida na ukivitumia unaongezeka uzito ndani ya muda mfupi sana.unaweza kuwasiliana na sisi ukivihitaji.

Tumia sahani kubwa wakati wa kula; sahani kubwa itakufanya upakue chakula kingi sana na kukupa nafasi ya kula sana tofauti na kutumia sahani ndogo ambayo hukubana kula.

Pata usingizi wa kutosha; usingizi ni muhimu sana kwa ukuaji wa misuli ya binadamu.

Kula mboga za majani na matunda mwisho wa mlo; mboga za majani  na matunda hupunguza uzito hivyo ukila mwanzoni zijaza nafasi tumboni na kumaliza nafasi ya vyakula vingine.

Acha ulevi wa pombe na sigara; tabia hizi hupunguza sana lishe ya mwili na kumfanya mtu ashindwe kuongezeka uzito.

Mwisho; shughuli ya kuongeza uzito sio rahisi kama jinsi shughuli ya kupunguza uzito...uzito unaongezeka taratibu ndani ya muda fulani na ukiamua kuongezeka uzito unatakiwa ujipe angalau miezi mitatu kwenda mbele kulingana na kilo unazotaka kuongeza na ili kupata moyo wa kuendelea basi  pima uzito angalau kila wiki kuona maendeleo.