Mwanamke amcharaza mumewe hadharani

 Mwanamke huyo aliyeonekana kupandwa na mori Jumatatu Agosti 29, alimcharaza mumewe hadharani Jijini Nairobi

– Mwanamke huyo alidai mumewe alikataa kurejea nyumbani wikendi na kwamba alikuwa amezima simu yake

Mwanamke alimcharaza mumewe hadharani Tom Street Jumatatu Agosti 29, 2016 mbele ya umma.

Wawili hao walikuwa wakigombana kwa sauti kubwa walipokuwa wakitembea katika barabara hiyo.

Walioshuhudia kisa hicho walisema mwanamke huyo alikuwa akimpigia kelele mumewe ambapo kiini cha mgogoro huo kilisemekana kuwa mwanamume huyo hakufika nyumbani wikendi.

Huku akiwa amekumbatia sketi yake katikati ya miguu, mwanamke huyo alimtukana kwa kumwita majina machafu na kumshutumu kwa kumpa magonjwa ya zinaa.

Alidai kuwa mumewe hakufika nyumbani wikendi na alikuwa amezima simu.


Kwa kujitetea, mwanamume huyo alidai kuwa alikamatwa akielekea nyumbani na aliachiliwa asubuhi hiyo. Hakuwa na simu, mshipi au viatu baada ya kuchukuliwa alipoingizwa seli, alisema.