O'Brien:Hali ya usalama ni tete mjini Aleppo nchini Syria

Mratibu wa umoja wa mataifa ametoa onyo juu ya hali ya kiusalama mjini Aleppo nchini Syria ambapo hali hiyo inahatarisha usalama wa kibinadamu.

Mratibu huyo wa misaada Stephen O'Brien amesema dunia haikuangalia wakati hospitali zikilipuliwa.

Ameomba baraza la usalama la umoja wa mataifa kupewa masaa 48 ya kusimamisha mapigano kwa ajili ya usambazaji wa misaada.

Katika maeneo mengine nchini Syria wapiganaji wa kikurdi wameishutumu serikali iliyopita inayoshikilia mji wa jirani wa Hasaka.