Rais Dkt. Magufuli apokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wa nchi mbalimbali ikulu jijini Dar leo

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Italia hapa nchini Roberto Mengoni Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea hapa nchini Kim Yong Su mara baada ya kupokea Hati zake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Somalia hapa nchini Mohammed Hassan Abdi mara baada ya kuwasili Ikulu kwa ajili ya kuwasilisha Hati zake za Utambulisho.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ireland hapa nchini Paul Sherlock Ikulu jijini Dar es Salaam.