Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki aondoka hospitalini

Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki

Aliyekuwa rais wa Kenya Mwai Kibaki, ambaye amekuwa akipokea matibabu nchini Afrika Kusini kwa kipindi cha wiki moja, ameruhusiwa kuondoka hospitalini.

Taarifa kutoka kwa familia yake Jumanne ilisema kiongozi huyo wa zamani "yupo katika hali nzuri".
Rais mstaafu wa Kenya Kibaki alazwa Afrika Kusini

Hata hivyo, ataendelea kukaa nchini Afrika Kusini kwa muda akiendelea kupata nafuu kabla yake kurejea Kenya.

Rais Kibaki alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Netcare Sunninghill kuondoa damu iliyokuwa imeganda kwenye mshipa wa shingoni siku chache baada ya kulazwa.