Inspekta Haroun aeleza kinachowakwamisha wasanii wakongwe

Msanii mkongwe wa muziki aliyewahi kuwa member wa Kundi la Gangwe Mob, Inspekta Haroun amefunguka na kueleza sababu mbalimbali zinazowafanya wasanii wakongwe kushindwa kufanya vizuri kama zamani.

Akiongea na Bongo5 wiki hii, Inspekta amesema hakuna ugumu kwa msanii mkongwe kufanya vizuri katika kipindi hiki ila muziki wao umekuwa na changamoto kadhaa.

“Muziki hauna mipaka kusema huyu mkongwe huyu wa sasa, yaani hata mimi leo nikiandaa ngoma yangu nzuri pamoja na video nitarudi vizuri tu. Unatakiwa uandae kitu kuanzia chini, watu wanataka kutengeneza tu video kali no, zalima audio iwe kali ili video ije kufanya vizuri zaidi,” alisema Inspekta.

Aliongeza, “Mashabiki wa muziki ni wale wale, wapo wanaopenda bongofleva ya sasa hivi na wapo wanaopenda bongofleva ya zamani, kwa hiyo haijalishi ukifanya kitu kizuri uwe mkongwe uwe mwanamuziki wa sasa utasimama. Kwa hiyo mimi nachozungumzia umakini na utendaji mzuri wa kazi na kuwa mbunifu katika utendaji wako unaweza ukasimama vizuri kabisa sina shaka na hilo.

Ingekuwa hivyo mimi tayari ningekuwa nishakata tamaa na kusema niache muziki wenyewe kwa sababu ndoto za kusimama tena kwenye chati hazipo, lakini imani yangu inaniambia kwamba naweza kusimama vizuri kabisa Inspekta kama Inspekta na watu wangu bado wapo na wananikubali sana,”

Miezi michache iliyopita Inspekta Haroun alidai kuwa alianza kufikiria biashara nyingine ya kufanya baada ya kutoa nyimbo takriban 20 na zote zikapotea hivi hivi, lakini baadaye alifanyiwa cancelling na familia yake nakurudi tena katika mapigano.